Raymond: Sina tatizo na Harmonize


Raymond amefafanua kinachoendelea kati yake na Harmonize kutokana na maneno yaliyoanza kuzungumzwa mtaani kuwa Harmonize ameanza kumkunjia Raymond.
12965173_229860914045895_485351563_n
Raymond12965173_229860914045895_485351563_n

 kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake‘Natafuta Kiki’kwenye redio na mtaani japo hauna muda mrefu tangu auachie. Akiongea kwenye kipindi cha 5 Selekt, kinachoruka kupitia EATV, Raymond alisema yeye na Harmonize hawana tatizo lolote na kila mtu anafanya muziki wake.
“Harmonize anafanya muziki mzuri, mimi hiyvo najitahidi kidogo watu wanasema nafanya vizuri. Lakini wote tunafanya muziki, Harmonize ana nyimbo zake nyingi nzuri ambazo nazijua ambazo najua watu hawazijui,” alisema Raymond.
Aidha Raymond aliongeza kuwa yeye na Feza Kessy ni washkaji tu hakuna kingine kinachoendelea.

Comments