Nyota huyu wa Hispania atasajiliwa na Man City ndani ya saa 24 zijazo.

Kama taarifa toka kwa rais wa Sevilla Jose Maria Del Nido ni za kuaminika basi mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Alvaro Negredo atakuwa mchezaji mpya wa Manchester City mpaka kufikia kesho saa kama hizi . Hii ni baada ya rais huyo kuthibititsha kuwa klabu yake ya Fc Sevilla na Manchester City zimefikia makubaliano juu ya mauzo ya mshambuliaji huyo ambapo ada yake ya uhamisho itakuwa paundi milioni 24.5 .
Dili la usajili wa mchezaji huyu lingeweza kukamilika mapema zaidi lakini Sevilla na City zilishindwa kufikia makubaliano ya bei halishi ya mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 .
Usajili wa Negredo utakapokamilika utafanya idadi ya wachezaji walioko kwenye kikosi cha kwanza cha City ambao ni raia wa Hispania kufikia wachezaji watatu baada ya David Silva ambaye atakuwa anaichezea City kwenye msimu wake wa tatu na Jesus Navas ambaye alisajiliwa mapema majira haya ya joto akitokea huko huko anakotoka Negredo Sevilla .
Ujio wa Negredo ambaye alifunga mabao 31 kwenye michuano yote akiwa na Sevilla msimu uliopita huenda ukamfanya mshambuliaji Edin Dzeko kuangalia uwezekano wa kuondoka kwani utafanya nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha City kuwa finyu zaidi.
Jembe jipya la City Alvaro Negredo.
                                                           Alvaro Negredo.

Comments

Post a Comment