Posts

Rais wa afrika kusini Cyril Ramaphosa amjibu Donald Trump

Image
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amemjibu Rais wa Marekani wa wakati huo, Donald Trump, baada ya Trump kutangaza kusitisha misaada kwa taifa hilo akidai kuwa kuna ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na madai kuwa Wazungu wananyanyaswa na kupokonywa ardhi wanazomiliki. Akijibu madai hayo, Ramaphosa amemtaka Trump aache kuingilia masuala ya ndani ya Afrika Kusini kwa kuwa hayamhusu. Amesisitiza kuwa ardhi ya Afrika Kusini ni ya raia wa nchi hiyo, na Trump hana mamlaka ya kuwapangia cha kufanya. “Hii ni ardhi yetu, sijui Donald Trump anahusika vipi au atafanya nini kuhusu ardhi ya Afrika Kusini kwa sababu hajawahi kuwa hapa. Aitunze Marekani yake, nasi tutaitunza Afrika Kusini yetu. Afrika Kusini ni ardhi yetu na inamilikiwa na watu wote wanaoishi hapa, siyo ya Trump,”...

Fabrizio Romano adai kutilia mashaka kurudi mara moja kwa Mykhailo Mudryk kwenye Soka

Image
Mwanasoka mashuhuri wa ndani Fabrizio Romano, sauti inayoaminika katika ulimwengu wa habari za uhamisho, ameweka shaka juu ya mustakabali wa hivi karibuni wa mwanasoka wa Ukrain Mykhailo Mudryk huku kukiwa na kashfa yake ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli. Akitumia jukwaa lake la mtandao wa kijamii X (zamani Twitter), Romano alionyesha mashaka juu ya matarajio ya Mudryk kurejea uwanjani hivi karibuni. “Kuhusu mtihani wa Mudryk… Kufikia sasa, kuna uwezekano mdogo sana kwamba Mykhailo ataweza kurejea kwenye soka siku za usoni,” Romano alifupisha kwa ufupi, kulingana na taarifa zilizopo kwa sasa. Hali hiyo inatokana na kipimo cha dawa za kuongeza nguvu mwilini ambacho kilifichua athari za dutu iliyopigwa marufuku ya meldonium. Matokeo ya uchambuzi wa “B-sampuli”...

Beyoncé atoa dola milioni 2.5 kusaidia waathiriwa wa moto Los Angeles

Image
Mwanamuziki mashuhuri na mrembo Queen Bey kupitia Taasisi Yake, Iitwayo “BeyGood”, Imeripotiwa Kuchangia Kiasi Cha $2.5m (Tsh Bilioni 6.3/=) Ili kusaidia Walioathirika na moto mkubwa unaoendelea huko Los Angeles. BeyGood, Imelenga kuwapa wahanga misaada ya dharura, kama vile chakula, malazi, na huduma za afya ya akili, huku pia ikisaidia miradi ya ujenzi na vitu vingine vingi . Hatua hii ni mfano wa jinsi mastaa na mashirika yao wanavyoweza kutumia ushawishi wao kusaidia watu walioko kwenye hali ngumu. Beyoncé amekuwa akisisitiza umuhimu wa kusaidia jamii zilizo na uhitaji mkubwa kupitia Mashirika na kampeni mbalimbali, na mchango huu unadhihirisha dhamira yake ya kusaidia wale walioko katika wakati mgumu.

WAJIPANGA NA OFA KWA MKONGWE WA MAN UTD ERIKSEN

Image
  Fenerbahce inamwinda kiungo wa kati wa Manchester United Christian Eriksen. Kando na kandarasi mwezi Juni, Eriksen anatarajiwa kuhamishwa na meneja mpya wa United Ruben Amorim mwaka ujao – na pengine mapema Januari. Fanatik anasema Fener ana shauku, ambapo kocha Jose Mourinho angemkaribisha Istanbul. Kwa upande wake, Eriksen hakati tamaa kubaki na United na anatarajia kupewa nafasi na Amorim kumshinda. Fener, wakati huo huo, wako tayari kutoa ofa ya Januari kwa raia wa Denmark kwa Mwaka Mpya na kushinikiza United kumuuza .

RAISI WA URUSI PUTIN AAHIDI MSAADA NCHI ZA KIAFRICA

Image
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa kile alichokiita “uungaji mkono kamili” kwa Afrika, ikiwa ni pamoja na katika mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali. Hotuba hiyo ilisomwa katika mkutano wa kilele katika eneo la mapumziko la Bahari Nyeusi huko Sochi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov kwa viongozi wenzake wa Afrika. Serikali kadhaa za Kiafrika zimekata uhusiano na washirika wa jadi wa Magharibi na wanatafuta msaada kwa Moscow katika kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajihadi. Wakati wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Karamoko Jean-Marie Traoré alisema Urusi ilikuwa mshirika wa kimataifa anayefaa zaidi kuliko mkoloni wa zamani, Ufaransa. Ni maoni yaliyotolewa na makoloni kadhaa ya zamani ya Ufaransa na yalitolewa tena n...

Hospitali 17 pekee Gaza zinafanya kazi ya kutoa huduma

Image
  Michael Ryan, Mkurugenzi wa Dharura za Kimataifa katika Shirika la Afya Duniani (WHO), ametangaza leo kwamba hospitali 17 pekee kati ya 36 Huko Gaza zinafanya kazi kwa sehemu kadhaa kutokana na mashambulizi ya Israel yanayoendelea. Katika majadiliano mtandaoni kuhusu hali ya afya huko Gaza, Ryan alisisitiza kwamba hospitali hizi zinakumbana na changamoto kubwa kutokana na uharibifu wa miundombinu, uhaba wa mafuta, upungufu wa vifaa vya matibabu, na uhaba wa wahudumu wa afya. Ryan pia aliripoti athari kubwa kwa huduma za afya, ambapo WHO imeandikisha mashambulizi 1,098 dhidi ya vituo vya afya katika maeneo ya Palestina yaliyo chini ya utawala wa Israel kati ya Oktoba 7, 2023, na Agosti 22, 2024. Kati ya mashambulizi haya, 492 yalitokea Gaza na kusababisha vifo 747 na majeruhi 969. Uharibifu huu umekandamiza sana mfumo wa afya wa Gaza, huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuzidi kuwa mbaya katika eneo hilo.

2020 MTV EMA NOMINEES LIST

Image
Ready, set,  VOTE ! The nominations for the 2020 MTV EMA are finally here and WOW… the competition is UNREAL at this year's show!   Lady Gaga is leading the nominations with nods in a whopping 7 categories! No surprises there: as if you didn't already know, 2020 is the year of Chromatica and we are so here for it! Following closely behind Gaga is a tie between Justin Bieber and BTS, each with 5 nominations!   Of course, we can't forget about the new additions to this year's category lineup! The 2020 MTV EMA will include three new awards: "Best Latin," "Video for Good" and "Best Virtual Live."   As always, the awards will go to the artists who get the most votes and it's up to the fans to vote for their favourites on mtvema.com and through social media.   Get ready for an awesome night of music – the show will be airing globally on Sunday, November 8, 2020. It's going to be one wild ride and trust us, you do NOT want to miss it!   Re...

WALIOVAMIA MADUKA YA WESTGATE ,HUKUMU KUTOLEWA LEO

Image
  Hukumu ya washukiwa wa mlipuko wa kigaidi katika jengo kubwa la maduka la Westgate jijini Nairobi mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 67 inatarajiwa kutolewa leo Jumanne baada ya kuahirishwa jana. Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amesema kuna mambo yalikuwa hajakamilika, na hivyo kulazimika kuahirisha uamuzi huo kwa mara nyingine. Watu 67 waliuawa katika shambulio hilo ambalo wanamgambo wa kundi la al-Shabab walidai kulitekeleza. Kundi la Al-Shabab linaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kanda hii kutokana na jinsi limekuwa likibadilisha mbinu ya mashambulizi katika taifa jirani la Somalia ambalo ndio chimbuko lao.

Dully sykes ft Maua sama :: Naanzaje

Image

WARAKA MPYA PAPA ACHAPISHA ; ''SOTE NI NDUGU TUSHUGHULIKIE MATATIZO ''

Image
  Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amechapisha Waraka mpya wa Kitume, akitoa wito wa kuwepo mshikamano katika jamii ili kuweza kuyashughulikia matatizo ya ulimwengu. Katika waraka huo wa Kipapa uliopewa jina ”Fratelli Tutti”, yaani ”Sote ni Ndugu,” na kutolewa jana katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican City umezikosoa sera za kinadharia kuhusu soko la kibepari kama suluhisho pekee la matatizo ya dunia. Papa Francis amegusia matatizo ya dunia kama vile mabadiliko ya tabia nchi, dhuluma zinazosababishwa na ukosefu wa usawa wa kiuchumi, tatizo la wahamiaji na janga la virusi vya corona. Waraka wa Kitume ni moja ya njia ya mawasiliano muhimu ya Papa na hutumika kama msingi wa mafundisho ya Kanisa Katoliki kwa kuangazia msimamo kuhusu masuala muhimu.

Manchester attack: Saffie Roussos mum 'told of her death'

Image
Image copyright PA Image caption Saffie Roussos, eight, was at the concert with her mother and older sister The mother of the youngest victim of the Manchester attack has been taken off life support and told about her daughter's death, the BBC understands. Eight-year-old Saffie Roussos, from Leyland, Lancashire, was one of the  22 people killed  at the Ariana Grande concert at Manchester Arena on 22 May. She was there with her mother, Lisa, and older sister Ashlee Bromwich. Family friend Mike Swanny said Mrs Roussos and Ms Bromwich were still in hospital but both "out of any danger".

Davido kuachia kitu kipya Ijumaa hii

Image
Baada ya kufanya vizuri na wimbo wa ‘If’ Davido amepanga kuachia kazi yake mpya Ijumaa hii. Muimbaji huyo wa Nigeria amethibitisha kuachia video yake mpya ya wimbo uitwao ‘Fall’ siku hiyo iliyotajwa hapo juu ambapo video hiyo imeongozwa na Daps. “FALL 02/06/17,” ameandika msanii huyo katika mtandao wake wa Instagram. Wakati huo huo Davido ni miongoni mwa wasanii watano kutoka Afrika wanaowania tuzo ya BET katika kipengele cha Best International Act: Africa ambapo anachuana na Wizkid, Tekno, Mr Eazi (wote kutoka Nigeria), Stonebwoy (Ghana), na Nasty C, Babes Wodumo na AKA (wote kutoka Afrika Kusini).

Rais Magufuli aagiza TCRA kuzifuta kampuni za simu zitakazoshindwa kujiunga na DSE

Image
Rais John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoyapiga faini makampuni ya simu atakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) badala yake wayafute. Rais Magufuli amesema hayo leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki. “Tulitangaza makampuni ya simu yajiunge na DSE na yamejizungusha na ni Vodacom pekee walijiunga. Makampuni ya simu kama mnajiamini kuwa mnalipa kodi, mnaogopa nini kujiunga na DSE tuone mapato yenu? TCRA, makampuni ya simu ambayo hayajajiorodhesha DSE msiyapige faini, yafuteni. Ni lazima tutoe maamuzi hata kama yanauma,” alisisitiza Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli ameyataka makampuni ya simu na mabenki kujisajili kwenye mfumo huo ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za serikali kwa uharaka na uaminifu zaidi. Na Emmy Mwaipopo

GoodNews: A.K.A wa South Africa kapata dili la kuperform main Stage ya BET

Image
Tuzo za  BET  ni tuzo kubwa za muziki kutoka Marekani na zenye heshima kubwa duniani, ambapo mwaka huu zitafanyika June 26 2016  Los Angeles  Marekani. Kama kawaida wasanii wataperform ila good news ni kutoka kwa rapper A.K.A kutoka South Africa ambaye nae anaingia katika histori ya msanii wa Afrika kupata nafasi ya kuperform kwenye main stage. Sambamba na A.K.A wasanii wengine watakaofanya perfomance siku hiyo ni pamoja na Rapper  Fat Joe, Lil Wayne   ,2chainz,   Fetty Wap ,  Desiigner  na wengine wengi.  A.K.A atakuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kuperform kwenye Main stage ya tuzo za BET ikiwa inaashiria kiasi gani muziki wa Africa unazidi kufanya vizuri duniani. A.K.A atafanya show kwenye  tuzo za BET June 25 2016,yaani siku moja kabla ya tuzo zenyewe kufanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater, hii ni good news nyingine kwa muziki wa Afrika baada ya siku chache Chris Brown kumualika Wizkid katika tour...

Maisha Plus 2016 yaja kivingine

Image
Mashindano ya Maisha Plus ambayo yamefahamika kwa kuwa na uhalisia zaidi yamerudi katika awamu nyingine tena. Majaji wa shindano hilo, Masoud Kipanya na Kaka Bonda Msimu huu mpya tutegemee ushindani mkubwa zaidi kutokana na wigo wa mashindano hayo kuwa kujikita katika nchi 5 za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya,Uganda,Rwanda,Burudi na wenyeji Tanzania. Usaili wa Mtwara ulivyokuwa Maisha Plus 2016 itakuwa inaruka katika runinga ya Azam Two kuanzia saa 3:00 usiku mpaka saa 4:00 usiku Na usahili ulianza June 4, mkoani Mtwara. Mashindano hayo msimu huu yamekuja na donge nono kwa mshindi kwani atajinyakulia kitita cha shilingi za kitanzania milioni 30

Diamond afunguka kuhusu Wema Sepetu wa sasa

Image
Tangu waachane ni kwa muda mrefu Diamond na Wema Sepetu wamekuwa kama paka na panya. Hali imeonekana kuwa tofauti kidogo siku za hivi karibuni baada ya Wema Sepetu kuchukua hatua na kuonekana kuanza kumsupport ex wake huyo ikiwa ni pamoja na kumuombea kura kwenye shindano la BET. Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, kinachoruka kupitia EATV, Diamond alisema, “Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekua labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa.” “Lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita,” aliongeza

Raymond: Sina tatizo na Harmonize

Image
Raymond amefafanua kinachoendelea kati yake na Harmonize kutokana na maneno yaliyoanza kuzungumzwa mtaani kuwa Harmonize ameanza kumkunjia Raymond. Raymond  kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake‘Natafuta Kiki’kwenye redio na mtaani japo hauna muda mrefu tangu auachie. Akiongea kwenye kipindi cha 5 Selekt, kinachoruka kupitia EATV, Raymond alisema yeye na Harmonize hawana tatizo lolote na kila mtu anafanya muziki wake. “Harmonize anafanya muziki mzuri, mimi hiyvo najitahidi kidogo watu wanasema nafanya vizuri. Lakini wote tunafanya muziki, Harmonize ana nyimbo zake nyingi nzuri ambazo nazijua ambazo najua watu hawazijui,” alisema Raymond. Aidha Raymond aliongeza kuwa yeye na Feza Kessy ni washkaji tu hakuna kingine kinachoendelea.

Video: Makomando – Sasanuvo

Image

VideoMPYA: Madee katuletea hii video mpya ya ‘migulu pande’ , ndani yumo Kajala na StanBakora

Image
Ni hit single ya mkali kutokea  Tiptop Connection  na ametimiza ahadi kama alivyosema, director ni Mtanzania  Adam Juma … ukishaitazama hii video hapa chini usiache kutoa comment yako maana  Madee  atapita kujua raia wake wameipokeaje.

PICHA & VIDEO: Diamond Platnumz kabomoa nyumba yao ya zamani Tandale DSM na kuijenga hii mpya.

Image
Hiyo picha hapo juu ni muonekano wa nyumbani anakotokea  Diamond Platnumz alikolelewa toka anakua.. panaitwa  Tandale  kwenye jiji la Dar es salaam ambapo staa huyu amepakumbuka siku zote na alitumia pesa zake kupatengeneza upya kama inavyoonekana kwenye  hii video fupi chini baada ya hii picha.