RAISI WA URUSI PUTIN AAHIDI MSAADA NCHI ZA KIAFRICA
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa kile alichokiita “uungaji mkono kamili” kwa Afrika, ikiwa ni pamoja na katika mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali. Hotuba hiyo ilisomwa katika mkutano wa kilele katika eneo la mapumziko la Bahari Nyeusi huko Sochi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov kwa viongozi wenzake wa Afrika. Serikali kadhaa za Kiafrika zimekata uhusiano na washirika wa jadi wa Magharibi na wanatafuta msaada kwa Moscow katika kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajihadi. Wakati wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Karamoko Jean-Marie TraorĂ© alisema Urusi ilikuwa mshirika wa kimataifa anayefaa zaidi kuliko mkoloni wa zamani, Ufaransa. Ni maoni yaliyotolewa na makoloni kadhaa ya zamani ya Ufaransa na yalitolewa tena n