Posts

WALIOVAMIA MADUKA YA WESTGATE ,HUKUMU KUTOLEWA LEO

Image
  Hukumu ya washukiwa wa mlipuko wa kigaidi katika jengo kubwa la maduka la Westgate jijini Nairobi mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 67 inatarajiwa kutolewa leo Jumanne baada ya kuahirishwa jana. Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amesema kuna mambo yalikuwa hajakamilika, na hivyo kulazimika kuahirisha uamuzi huo kwa mara nyingine. Watu 67 waliuawa katika shambulio hilo ambalo wanamgambo wa kundi la al-Shabab walidai kulitekeleza. Kundi la Al-Shabab linaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kanda hii kutokana na jinsi limekuwa likibadilisha mbinu ya mashambulizi katika taifa jirani la Somalia ambalo ndio chimbuko lao.

Dully sykes ft Maua sama :: Naanzaje

Image

WARAKA MPYA PAPA ACHAPISHA ; ''SOTE NI NDUGU TUSHUGHULIKIE MATATIZO ''

Image
  Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amechapisha Waraka mpya wa Kitume, akitoa wito wa kuwepo mshikamano katika jamii ili kuweza kuyashughulikia matatizo ya ulimwengu. Katika waraka huo wa Kipapa uliopewa jina ”Fratelli Tutti”, yaani ”Sote ni Ndugu,” na kutolewa jana katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican City umezikosoa sera za kinadharia kuhusu soko la kibepari kama suluhisho pekee la matatizo ya dunia. Papa Francis amegusia matatizo ya dunia kama vile mabadiliko ya tabia nchi, dhuluma zinazosababishwa na ukosefu wa usawa wa kiuchumi, tatizo la wahamiaji na janga la virusi vya corona. Waraka wa Kitume ni moja ya njia ya mawasiliano muhimu ya Papa na hutumika kama msingi wa mafundisho ya Kanisa Katoliki kwa kuangazia msimamo kuhusu masuala muhimu.

Manchester attack: Saffie Roussos mum 'told of her death'

Image
Image copyright PA Image caption Saffie Roussos, eight, was at the concert with her mother and older sister The mother of the youngest victim of the Manchester attack has been taken off life support and told about her daughter's death, the BBC understands. Eight-year-old Saffie Roussos, from Leyland, Lancashire, was one of the  22 people killed  at the Ariana Grande concert at Manchester Arena on 22 May. She was there with her mother, Lisa, and older sister Ashlee Bromwich. Family friend Mike Swanny said Mrs Roussos and Ms Bromwich were still in hospital but both "out of any danger".

Davido kuachia kitu kipya Ijumaa hii

Image
Baada ya kufanya vizuri na wimbo wa ‘If’ Davido amepanga kuachia kazi yake mpya Ijumaa hii. Muimbaji huyo wa Nigeria amethibitisha kuachia video yake mpya ya wimbo uitwao ‘Fall’ siku hiyo iliyotajwa hapo juu ambapo video hiyo imeongozwa na Daps. “FALL 02/06/17,” ameandika msanii huyo katika mtandao wake wa Instagram. Wakati huo huo Davido ni miongoni mwa wasanii watano kutoka Afrika wanaowania tuzo ya BET katika kipengele cha Best International Act: Africa ambapo anachuana na Wizkid, Tekno, Mr Eazi (wote kutoka Nigeria), Stonebwoy (Ghana), na Nasty C, Babes Wodumo na AKA (wote kutoka Afrika Kusini).

Rais Magufuli aagiza TCRA kuzifuta kampuni za simu zitakazoshindwa kujiunga na DSE

Image
Rais John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoyapiga faini makampuni ya simu atakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) badala yake wayafute. Rais Magufuli amesema hayo leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki. “Tulitangaza makampuni ya simu yajiunge na DSE na yamejizungusha na ni Vodacom pekee walijiunga. Makampuni ya simu kama mnajiamini kuwa mnalipa kodi, mnaogopa nini kujiunga na DSE tuone mapato yenu? TCRA, makampuni ya simu ambayo hayajajiorodhesha DSE msiyapige faini, yafuteni. Ni lazima tutoe maamuzi hata kama yanauma,” alisisitiza Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli ameyataka makampuni ya simu na mabenki kujisajili kwenye mfumo huo ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za serikali kwa uharaka na uaminifu zaidi. Na Emmy Mwaipopo

GoodNews: A.K.A wa South Africa kapata dili la kuperform main Stage ya BET

Image
Tuzo za  BET  ni tuzo kubwa za muziki kutoka Marekani na zenye heshima kubwa duniani, ambapo mwaka huu zitafanyika June 26 2016  Los Angeles  Marekani. Kama kawaida wasanii wataperform ila good news ni kutoka kwa rapper A.K.A kutoka South Africa ambaye nae anaingia katika histori ya msanii wa Afrika kupata nafasi ya kuperform kwenye main stage. Sambamba na A.K.A wasanii wengine watakaofanya perfomance siku hiyo ni pamoja na Rapper  Fat Joe, Lil Wayne   ,2chainz,   Fetty Wap ,  Desiigner  na wengine wengi.  A.K.A atakuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kuperform kwenye Main stage ya tuzo za BET ikiwa inaashiria kiasi gani muziki wa Africa unazidi kufanya vizuri duniani. A.K.A atafanya show kwenye  tuzo za BET June 25 2016,yaani siku moja kabla ya tuzo zenyewe kufanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater, hii ni good news nyingine kwa muziki wa Afrika baada ya siku chache Chris Brown kumualika Wizkid katika tour...